biashara school

Jinsi ya Kuanzisha Mfumo wa Hesabu za Biashara Ndogo

Wafanyabiashara wengi huanza biashara kwa nguvu, lakini bila mfumo rasmi wa hesabu za biashara. Mwanzoni inaweza kuonekana rahisi – kuandika mauzo kwenye daftari au kukariri kichwani. Lakini kadri biashara inavyokua, kutokuwa na mfumo wa mahesabu huanza kuleta hasara.

Mfumo wa hesabu za biashara sio kwa makampuni makubwa pekee. Ni kwa kila mfanyabiashara mdogo anayehitaji udhibiti wa fedha na faida.

Katika makala hii, utajifunza jinsi ya kuanzisha mfumo wa hesabu kuanzia sifuri.


Hatua ya 1: Tenganisha Fedha za Biashara na Fedha Binafsi

Hii ndio msingi.

Usichanganye:

  • Mauzo ya biashara
  • Pesa ya matumizi ya nyumbani

Fungua:

  • Akaunti ya biashara (ikiwa inawezekana)
    AU
  • Bahasha/box tofauti kwa pesa za biashara

Bila hatua hii, huwezi kujua faida halisi.


Hatua ya 2: Anzisha Mfumo wa Kurekodi Mauzo

Chagua mfumo rahisi lakini thabiti:

  • Daftari la mauzo
  • Excel
  • Mfumo wa kidijitali

Rekodi:

  • Tarehe
  • Bidhaa
  • Bei
  • Kiasi
  • Jumla

Rekodi kila siku. Usisubiri mwisho wa wiki.


Hatua ya 3: Rekodi Matumizi Yote

Wafanyabiashara wengi huandika mauzo tu.

Lakini faida hupatikana baada ya kutoa matumizi.

Rekodi:

  • Gharama za manunuzi ya stock
  • Kodi
  • Umeme
  • Usafiri
  • Mishahara

Hata matumizi madogo ni muhimu.


Hatua ya 4: Fanya Hesabu ya Faida Kila Wiki au Mwezi

Faida = Mapato – Matumizi

Bila kufanya hesabu hii mara kwa mara, unaweza kudhani unapata faida wakati unapoteza.


Hitimisho

Kuanzisha mfumo wa hesabu za biashara sio jambo gumu. Kinachohitajika ni nidhamu.

Ikiwa unataka mfumo kamili, wa kitaalamu na unaoeleweka hatua kwa hatua, jiunge na Kozi ya Hesabu za Biashara na Usimamizi wa Kitaalamu ili ujifunze mfumo wa advanced unaokuwezesha kudhibiti fedha, stock na faida kwa uhakika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *