About Us
Lengo letu
Biashara School ni jukwaa la mafunzo ya biashara kwa Kiswahili, lililoundwa kuwawezesha wanawake kujenga na kukuza biashara kwa misingi sahihi, kwa utulivu, na kwa faida endelevu.
Inua Biashara yako kwa Kujielimisha wewe kwanza
Kozi za Biashara school nyenzo bora ya kukusaidia kufanya maamuzi bora, kuelewa biashara kwa ujasiri, na kujenga brand/biashara ya muda mrefu yenye faida.
Virginia Maenda.
Founder
Dira yetu
Biashara School
Kuwa taasisi inayoongoza Afrika Mashariki katika kuwajengea wanawake uwezo wa kitaalamu wa kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara zenye mifumo imara na endelevu.
Tunaamini kuwa FAIDA YA KUDUMU haiji kwa bahati- inatokana na MAARIFA sahihi, MAAMUZI ya kimkakati na MIFUMO inayotekelezeka. Kupitia mafunzo yaliyoandaliwa kitaalamu, tunawawezesha wanawake wamiliki wa biashara kuelewa FEDHA zao, kuboresha UENDESHAJI wa kila siku na kusimamia UKUAJI kwa utaratibu unaopimika.
Lugha ya Kiswahili
Kozi zetu hutumia Kiswahili rahisi na mazoezi ya vitendo ili kuhakikisha uelewa wazi na matumizi halisi kwa kila mshiriki.
Mitaala ya biashara
Tukijumuisha mada muhimu kama gharama, bei, na mauzo, tunakusaidia kupanga kwa ufanisi na kufanya maamuzi sahihi kwa mafanikio ya kudumu.
Jumuiya ya wajasiriamali
Jiunge na mtandao wa wanawake wanaojenga biashara kubwa kupitia mafunzo yetu.
